Kipimo cha CT Scan ni moja kati ya vipimo vya kisasa katika dunia ya leo. Kusini mwa Tanzania na kaskazini mwa msumbiji, takribani eneo la mraba lenye kilomita 500 kuzunguka hospitali bado hakuna huduma ya CT Scan.
Kwa wagonjwa wenye kiharusi au kutokwa na damu kwenye ubongo, uwimbe mbalimbali kama vile kansa na magonjwa mengine, CT scan ni muhimu kwa utambuzi wa kuaminika na upangaji wa tiba.
Kwa sababu ya uhitaji mkubwa ya uchunguzi huu, uongozi wa hospitali umeamua kufunga mashine ya CT scan mapema mwaka 2021.
Chumba cha kukinga mionzi lazima kipatikane. Kwa hiyo baadhi ya kazi za ujenzi upya ni muhimu katika idara yetu ya x-ray. Jumla ya gharama za mradi huu ikiwa ni pamoja na ujenzi, mashine ya CT Scan na UPS itagharimu 300.000 €. Hadi sasa tayari tumeshakusanya zaidi ya asilimia 90 ya fedha hii (Januari 2021) na ujenzi wa chumba cha kukinga mionzi tayari umeshaanza.