Wodi zetu zilijengwa kati ya mwaka 1965 na 1975. Kwa sasa hazikidhi mahitaji na viwango, madirisha yameharibika ,sehemu za paa zinavuja maji inyeshapo mvua,wagonjwa kukosa faragha, vyoo si rafiki kwa wenye ulemavu n.k. Mabomba ya kutiririsha maji ya mvua ni ya zamani sana na mengine yameziba na kusababisha mafuriko katika baadhi ya wodi inyeshapo mvua kubwa.
Ukararabati unahitajika kwa haraka, pamoja na mabomba ya maji ya mvua,ukarabati wa korido,kuweka vigae,na mwanga wa kutosha kwenye wodi na ujenzi wa vyoo rafiki kwa wenye ulemavu.
Mnamo Septemba 2021 hadi Desemba 2021, tumefanikiwa kukarabati wodi yetu ya upasuaji ya wanaume, choo kimoja na korido. Ndani ya wodi,vigae vimewekwa pamoja na madirisha na mapanzia mapya ili kuwa na faragha zaidi kwa wagonjwa wetu. Sakafu ya korido ya mlango mkubwa wameweka tarazo.
Shukrani kwa mchango wa ukarimu kupitia Missio Austria, tumefanikiwa kukarabati vyoo vya wodi ya upasuaji ya wanaume na wanawake na kukarabati mfumo wa maji ya mvua.
Kwa wodi 5 zilizobaki na vyoo wodi 3, mbunifu wetu anaboresha mipango na tutaendelea na ujenzi katika kipindi cha mwaka 2022.