Ndanda

Idara ya maabara

Jengo la maabara la Hospitali ya Rufaa ya Mtakatifu Benedict Ndanda lilijengwa mwaka 2015 chini ya mradi wa Mtandao wa Maabara ya Afya ya Umma Afrika Mashariki (EAPHLNP). Maabara ina sehemu sita ambazo ni Hematology, Blood Transfusion, Parasitology, clinical chemistry, Serology na Microbiology. Timu yetu ina wataalam 18 wenye uzoefu na bidi chini ya uongozi wa Sia Temu ambaye ana shahada ya uzamili ya microbiolojia, na epidermiolojia. Mashine mbadala  zimefungwa kwenye vifaa vyote muhimu. Kwa hiyo vipimo vyote vinapatikana bila usumbufu hata kasoro za kiufundi zikitokea.

Maabara yetu inachunguza zaidi ya vipimo 90 na kwa siku sampuli za wagonjwa wapatao 150 hadi 200 hupokelewa. Kwa jumla zaidi ya  vipimo 140,000 hupimwa kwa mwaka. Mara nyingi majibu yanapatikana katika mfumo wetu wa kielektroniki ndani ya saa moja hadi mawili baada ya sampuli kuchukuliwa. Kwa uchunguzi maalum tunashirikiana na Hospitali ya Taifa Muhimbili na kwa sampuli za biopsy tunashirikiana na Taasisi ya Saratani ya Msamaria Mwema Ifakara. Maabara imeidhinishwa kwa mujibu wa kiwango cha ISO 15189.