Ndanda

Historia

Mara baada ya vita ya majimaji 1905 wamisionari wabenediktini wa kijerumani toka mtakatifu otilia waliamua kuanzisha kituo kipya ndanda ambacho kilikuwa kama makao makuu ya kusini mashariki mwa nchi.

1905

Mara baada ya vita ya majimaji 1905 wamisionari wabenediktini wa kijerumani toka mtakatifu otilia waliamua kuanzisha kituo kipya ndanda ambacho kilikuwa kama makao makuu ya kusini mashariki mwa nchi.

1906

15/8/1906 wamisionari walipanda msalaba

1908

Mwaka 1908 wamisioanari masista wa mtakatifu bededicto walianza kuhudumia wagonjwa

1910

Mwaka 1910 ujenzi wa hospitali ndogo ya ndanda ulianza

1911

Ndanda from North-East in 1911. From left to right: Chapel, house of the brothers, mansions, school farm, kitchen, house of sisters. At the bottom, old hospital.

1912

Courtyard with mission cross in 1912

1916

Mwezi wa kumi 1916 wakati wa vita ya kwanza ya dunia hospitali ya jeshi ilifunguliwa ndanda

1917

Mwezi wa kumi na moja 1917 washirika wa ndanda walitekwa na wamisionari wakijerumani walifukuzwa nchini.

1925

Mwishoni mwa vita kuu ya kwanza ya dunia masista walirudi ndanda na mwezi wa sita 1925 huduma za wagonjwa zilirudi tena

1926

Mwaka 1926 majengo ya zamani yalibomolewa na kujengwa upya;Ujenzi ulikamilika rasmi mwaka 1927.Jengo hilo lipo hadi leo hii likijulikana kama private ward.

1927

Tarehe 5 mei 1927 sista Dkt Thecla Stinnesbeck OSB ambaye ni daktari (MD) pia mjumbe wa shirika la wamisionari aliwasili na kuanza kutibu wagonjwa.Alikuwa daktari wa kwanza kwa miaka ishirini 20 iliyopita.Alifuatia pia Sista Dkt Maria Lukas Rauch OSB ambaye aliwasili mwaka 1947.Baada ya hapo walifuata wengine.

1930

Tarehe 22/septemba/1930 Sista Dr Thecla alianzisha shule ya uuguzi ambayo ilifunguliwa na waziri wa elimu wakati ule.

1933

Mwaka 1933 Sr Thecla alianza kuwafundisha ukunga masista wenzake wamisionari

1940

Mwaka 1940 mafunzo ya ukunga yalianza kutolewa kwa wanawake walioolewa tu na wasioolewa ilikuwa marufuku.

1945

Mwishoni mwa vita kuu ya pili ya Dunia 1945 tayari hospitali ilikuwa na jumla ya vitanda 103.

1965

Chuo cha uuguzi ndanda kilianzishwa Mwaka 1965 kikiwa chini ya uangalizi wa Shirika la Mt Benedikto Ndanda.

1970

Mwaka 1970 wodi muhimu (W1-W8) zilifunguliwa rasmi na waziri wa Afya Mr Sijaona.

1977

Kwa mara ya kwanza ajira ilitolewa kwa madaktari wawili 2 wa kitanzania hii ilikuwa mwaka 1977 yaani alikuwa Dkt Mdeme (AMO) na Dkt David Mwambe (MD).

2004

Mwaka 2004 Jengo la upasuaji lilifunguliwa na Mkuu wa Mkoa Mh Isidor Shirima.Pia jengo la uchomaji taka lilijengwa 2004.

2010

Tarehe 12/Novemba/2010 Hospitali ilipandishwa hadhi na kuwa Hospitali ya rufaa kupitia walaka wa serikali Na828 na kutangwazwa kwenye gazeti la Serikali.

2013

Tarehe 04/Disemba/2013 Bweni la wasichana la shule ya uuguzi lilifunguliwa na Mh Askofu Gabriel Mmole wa Jimbo la Mtwara.

2014

Tarehe 28/03/2014 hatua za awali zilikamilika za ujenzi wa maabara ya kisasa,na jiwe la msingi liliwekwa na Naibu Waziri wa Afya na Ustawi wa Jamii Mh Dkt Stephen Kebwe (MP) Mbunge.