Ndanda

Kambi ya mguu kifundo 2023

Kuanzia tarehe 19/03/2023 hadi tarehe 02/04/2023, Daktari Ute Terheggen  na timu yake walitutembela  Ndanda.  Ni wataalamu maalum wa upasuaji wa mguu kifundo uliodharauliwa. Watoto walio na mguu kifundo wanaweza kutibiwa kwa kufunga kopa, ikiwa  matibabu yataanza mapema  siku chache au wiki baada ya kuzaliwa. Kwa wanaokuja wakiwa wamechelewa sana kwa njia hii ya kufunga kopa wanapaswa kutibiwa kwa upasuaji maalumu. Matangazo kuhusu kambi hii yalifanywa  kupitia vipeperushi na matangazo ya redio. Zaidi ya  Wagonjwa 70 walifika  na wote walipewa ushauri  na wataalamu.  

Madaktari 4  wa upasuaji wa mifupa, wataalamu wa usingizi wawili, wauguzi wawili wa chumba cha upasuaji na muuguzi mmoja wa dawa ya usingizi  kutoka Ujerumani. walishirikiana na wafanyakazi wetu. Wamefanikiwa  kufanya upasuaji wa kwa wagonjwa 35 bila matatizo yeyote. Baada ya muda wa upasuaji wagonjwa wataanza kutembea kama kawaida. Mradi huu umefadhiliwa na shirika la misaada linaloitwa  Pro Interplast  na huduma zote za upasuaji unafanywa bure bila malipo,ikiwemo kulazwa na chakula kwa wagonjwa.