Kuanzia tarehe 21/4/2022 hadi tarehe 23/4/2022, Dk. Winfried Grasbon, daktari bingwa wa macho kutoka Ujerumani ametutembelea tena Ndanda kwa mara tano na kwa mara ya 55 kwa Tanzania. Anaungwa mkono na timu yake ya uuguzi pamoja na wafanyakazi wa kliniki yetu ya macho, pamoja na madaktari watatu wanaomaliza taaluma ya opthalmology jijini Dar Es Salaam wanahudhuria kambi hii kupata uzoefu kwa vitendo. Dr Hussein Mjaliwa anafadhiliwa na hospitali yetu na atarejea baada ya kumaliza taaluma yake ifikapo mwishoni mwa mwaka huu.
Dk. Grasbon na timu yake wamefanikiwa kufanya upasuaji wa mtoto wa jicho 79 ndani ya wiki mbili. Wagonjwa walilipia ada ya shilingi 150,000 tu kwa huduma hii ya upasuaji, kulazwa na chakula. Wagonjwa wengi walikuwa na mtoto wa jicho na kutoona kabisa. Lakini baada ya upasuaji waliweza kuona tena. Kwa namna Dk. Grasbon anavyofanya kazi kwa bidii ushangaza sana na huvutia zaidi kwasababu ana umri usiopungua miaka 83.