Ndanda

Wodi ya watoto

Watoto chini ya miaka 12 wanalazwa kwenye wodi ya watoto. 
Madaktari bingwa wawili wa watoto, daktari moja (MD), madaktari wanaotarajiwa (Intern doctors) watano na manesi 22 wanahudumia wagonjwa hawa.

Kitengo kimefaulu kushughulikia matatizo ya moyo na yale ambayo yanashindikana mgonjwa hupewa rufaa ya kwenda hospitali ya Taifa Muhimbili ama Hospitali ya ocean Road Dar es Salaam kwa matibabu zaidi.Pia wamefaulu kushughulikia matatizo machache kama Sphingolipidosis ambayo huitaji tiba maalum za enzaim (vichocheo).

Tunatoa shukrani na Asante kwa Mradi wa Msamaha wa Tiba kwa Watoto. Hivi sasa tunatoa huduma za msamaha kwa watot wenye wazazi wasio na uwezo wa kugharamia matibabu.