Ndanda

Group picture

Makabidhiano ya Nyumba ya Wageni

Tarehe 19 mwezi wa pili mwaka 2024 nyumba ya wageni ilikabidhiwa na mkandarasi, Ujenzi ulianza mwezi wa tano mwaka 2023, kwa sasa ujenzi umeisha na jengo liko tayari kwa matumizi ya wageni wetu. Tunamshukuru msanifu wa majengo kwa kazi mzuri na ubunifu ,pia kwa mkandarasi kwa utekelezaji sahihi wakati wa ujenzi na kusababisha muonekano wa kuvutia wa jengo hili, Nyumba ya wageni hii itachangia kwa kiasi kikubwa katika kutatua changamoto yetu ya muda mrefu ya uhaba wa malazi kwa wageni kutoka nje,ambao hukaa nasi kwa muda maalum.

Nyumba ya kulala wageni ipo kando ya Barabara kuu kutoka hospitalini.Nyumba ya wageni mpya ina vyumba 10 vinavyojitegemea,eneo la mapokezi, jiko, eneo la chakula, uani, na chumba cha kufua nguo. Nyumba hii ni kwa ajili ya wageni wa hospitali kama wataalam wanaotutembelea kutoka nje. Tunatoa shukrani za dhati kwa wafadhili wetu wakarimu,ambao wamejitolea michango iliyofanikisha mradi huu. Asante kwa michango muhimu tuna maono ya pamoja ya kutoa kiwango cha juu cha huduma maalum zinazoweza kufikiwa na wote.