Ndanda

Kiujumla

Kitengo cha magonjwa ya ndani kinaongozwa na daktari bingwa pia ina madaktari wanne (MD), daktari msaidizi mmoja (AMO) na wanne waganga (CO) pamoja na madaktari wanafunzi watano.
Huduma za wagonjwa wa nje ni pamoja na wagonjwa binafsi na wa BIMA.

Pia tuna kliniki ya shinikizo la damu na moyo, kliniki ya kisukari, matatizo ya figo, kliniki ya magonjwa ya akili na ushauri Nasaha HIV- AIDS (CTC).

Kwa wagonjwa waliolazwa tuna wodi binafsi daraja la kwaza na la pili (Grade 1 and 2) na daraja la tatu ward 3 yakike and ward 4 yakiume.
Maabara yetu inahadhi ya nyota tano, na ndiyo hutumika kufanya vipimo mbalimbali. Pamoja na hivyo kuna vipimo vya ultrasound, ECG, X-ray na endoscopy.
Endoscopy ni kipimo cha kisasa kinachotumia kamera kuingia na kuona ndani ya tumbo na utumbo, pia kinatoa tiba kwa wagonjwa wenye tatizo la kutapika damu, wanaoshindwa kumeza, kutoka damu kwenye hajakubwa, na matatizo mengine ya mfumo wa chakula.

Tangu mwaka 2017 tunatoa huduma ya kuchungua damu na sehemu mbali mbali za mwili katika ngazi ya celi yaani cytology. Sampuli huchukuliwa kwa mgonjwa, kuandaliwa na kupigwa picha katita hospital yetu na baadae hutumwa kwa mtandao kwa wataalamu wa cytology kwaajili ya kusomwa na kupatiwa majibu. Njia hii huitwa telecytology.