Ndanda

Kliniki ya meno na kinywa

Idara hii ina Daktari mmoja 1 wakinywa, Daktari mmoja Msaidizi wa kinywa,Tabibu wa meno pamoja na mtaalamu/injinia wa meno,kitengo pia kina wasaidizi wanne 4.

Kwa wastani watu zaidi ya 90-100 kwa wiki hupata huduma na tiba za meno na kinywa. Gharama ya chini kwa huduma za meno ni tsh 10,000/=.Kutokana na ukuaji wa teknologia hivi sasa tunatoa huduma ya uzibaji meno. Pia tunauwezo wa kutibu taya na mifupa ya kinywa iliyo vunjika kutokana na ajali au sababu nyinginezo kitaalamu “leFort fracture”.Pia kitengo kina vifaa vya kisasa kama vile mashine ya x-ray ya kidigitali viti / vitanda vitano vyenye hazi ya juu vinavyotumika kwenye kutoa tiba za meno na kinywa,pamoja na Maabara ya meno.