Ndanda

Idara ya tiba na mazoezi ya viungo

Kitengo chetu cha fiziotherapia kina wataalamu wawili wa wa fiziotherapia na wasaidizi wawili. piaKinashughulikia wagonjwa wa nje na wandani,wastani wa wagonjwa 250 hupata huduma kwa mwezi.

Mtaalaamu wa fiziotherapia ana wajibu wa kuzuia na kutibu magonjwa mbalimbali ya viungo au ulemavu kwa kutumia vifaa tiba kama mashine maalum na vifaa vya kisasa kitaalamu; tissue manipulator, traction machines, TENS theraputic ultrasouns nad infrared therapy.

Elimu ya mazoezi ya viungo hutolewa kwa wagonjwa wenye maumivu ya mgongo iitwayo ergonomic education.

Kitengo kina kliniki maalum kila jumanne ya wiki kwa watoto wenye ulemavu wa miguu kifundo hasa wa umri chini ya miaka miwili 2 kwa kutumia njia ijulikanayo kama Ponseti treatment protocol.Na wale wenye umri zaidi ya miaka miwili hufanyiwa upasuaji na Daktari bingwa toka Ujerumani Dkt Fritjof.

Pia tunatoa huduma za urejeshaji kwa wagonjwa walio athirika na kiarusi,kupooza,matatizo ya uti wa mgongo,mivunjiko nk.