Ndanda

Kliniki ya macho

Kitengo cha macho kina idara tatu 3 nazo ni;Kliniki ya macho,Wodi ya macho,na chumba cha Upasuaji wa jicho.Kwa sasa kuna Manesi watatu 3 waliosomea magonjwa ya macho,Mafundi sanifu wa miwani wapo wawili 2 pamoja na Nesi Msaidizi mmoja 1.

Kitengo kinashughulikia shida za macho na utengenezaji wa miwani ,uchunguzi,na upasuaji mdogo wa macho kama vile viuvimbe vidogo vya macho kitaalamu Pterygiumexcision,BTRP na Evisceration.Kwa sasa kitengo kina mkakati wa kupunguza Upofu Nchini Tanzania kwa kufanya upasuaji wa mtoto wa jicho na Trabeculectomy mara mbili kwa mwaka.Upasuaji ambao hufanywa na daktari bigwa kutoka Ujerumani Dkt Winfried Grasbon