Hospitali ya rufaa ya Mtakatifu Benedicto ni hospitali binafsi ya kidini inayohudumiwa na wamisionari wa shirika la mtakatifu Benedicto wa mtakatifu Otilia wa Ujerumani.
Ni sehemu pia ya Abasia ya Ndanda iliyopo mkoani Mtwara,Kusini mashariki mwa Tanzania
Tangu kuanza kwa umisionari wa Mt. Benediktine Nchini Tanzania,ilikuwa wazi kuwa kuhudumia wagonjwa ilikuwa ni sehemu moja wapo katika utume wetu.
Lengo kuu ni kutoa huduma bora kwa wagonjwa bila kujali tofauti zao za kijamii na kiuchumi.
Tunatoa huduma za msingi kwa kutumia nyenzo na vifaa vya kisasa kabisa.Maabara yetu ni ya kisasa pia na inavifaa vya kutosha na ilishapata tuzo ya Nyota 5.Tuna x-ray ya kidigitali na mashine ya kisasa ya Ultrasound (U/S).
Kutokana na janga la kuenea kwa virusi vya Covid 19 duniani uongozi wa hospitali umeamua kujenga mtambo utakaozalisha hewa ya oxijeni.
Miradi iliyopewa kipaumbele kwa mwaka 2019/2020 ni ujenzi wa jengo la wagonjwa wanaohitaji uangalizi maalum,ikiwa ni pamoja na watoto wachanga (NICU) na huduma ya matibabu ya figo.
Kutokana na uhitaji mkubwa wa mashine hiyo uongozi wa hospitali ya ndanda imedhamilia kufunga mashine hiyo katika mwaka 2020.