Ndanda

CT Scan

Msamaha kwa Watoto

Shukrani zetu za dhati zifike kwa Daktari bingwa wa watoto Dr. Low kutoka Ujerumani, asante kwa msaada wa ukarimu, hospitali imetekeleza huduma ya ‘Msamaha kwa Watoto’. Watoto wote ambao wazazi wao wanashindwa kulipia huduma za vipimo na matibabu na kuthibitishwa na daktari wanafaidika na msaada huu.

Hadi sasa zaidi ya watoto 200 chini ya miaka 12 wamefaidika na mpango huu. Mwaka 2022 mwezi wa tatu, Kwa mfano, watoto wenye vidonda vikubwa vilivyosababishwa na ajari ya moto ambao wanahitaji upandikizwaji wa ngozi, watoto wenye majeraha makubwa kutokana na kuumwa na mamba, watoto wachanga wanaohitaji uangalizi maalum (NICU) au watoto wenye matatizo ya figo kushindwa kufanya kazi ambao wanahitaji huduma ya uchujaji damu.
Huduma ya uchujaji damu ni huduma ya kisasa na yenye gharama kubwa kutolewa kwenye taasisi yetu. Tunashukuru kwa mradi huu, ndani ya mwaka 2021, watoto watano (5) wametibiwa kwa mafanikio makubwa kwa huduma ya uchujaji damu kwa njia ya tumbo au uchujaji damu kwa njia ya damu.