Ndanda

Huduma ya CT Scan

Kipimo cha CT Scan ni moja kati ya vipimo vya kisasa katika dunia ya leo..Kusini mwa Tanzania na kaskazini mwa msumbiji , takribani eneo la mraba lenye kilomita 500 kuzunguka hospitali bado hakuna huduma ya CT Scan.

Kwa wagonjwa wenye kiarusi na shinikizo la damu,kuvuja damu kwenye ubongo na uvimbe kwenye ubongo wanahitaji CT Scanili waweze kupata uchunguzi na matibabu sahihi.

Kutokana na uhitaji mkubwa wa mashine hiyo uongozi wa hospitali ya ndanda imedhamilia kufunga mashine hiyo katika mwaka 2020.

Hospitali italazimika kuandaa chumba ambacho kitaweza kukinga na kuzuia mionzi ya CT Scan isitoke nje, hivyo basi ukarabati utahitajika kufanyika katika jengo lililopo la X ray (chumba cha mionzi)

Gharama zote zitakazotumika toka ujenzi , ununuaji wa mashine na kifaa cha kutunzia umeme (UPS) ni shiling milioni mia saba sabini na mbili laki moja ishirini na tatu mia moja kumina tatu bila sent .(772,123,113.00) tumeweza kuweka akiba ya asilimia sitini (60%)kufikia mwezi wa saba 2020.