Ndanda

Kitengo cha dawa

Kitengo cha dawa kwa sasa kina wafanyakazi saba 7 ambao wamepata mafunzo maalum ya ugawaji wa dawa. Ili kurahisisha upatikanaji huduma kitengo hiki kimewagawa wagonjwa katika makundi mawili yani wagonjwa wa BIMA na kawaida lengo likiwa ni kupunguza msongamano na kuharakisha huduma katika dirisha la dawa.

Kitengo kinauwezo wa kuhudumia watu kati ya 80-150 kwa siku tena kwa ufanisi wa hali ya juu bila kucheleweshwa wagonjwa.

Kitengo pia kinagawa dawa za mawodini na chumba cha upasuaji, kwa sasa dawa zote muhimu zinapatikana kwa gharama nafuu ambazo asilimia kubwa ya wagonjwa wanazimudu.