Ndanda

Kitengo cha Endoscopy

Kitengo chetu cha endoscopy kina mashine za kisasa ambazo hutumia camera inayowezesha kuingia katika tumbo, utumbo mdogo na utumbo mkubwa, pia inatuwezesha kuingina ndani ya mapafu, kwa kufanya hivi tunaweza kugundua matatizo mbali mbali na kutoa tiba panapo stahili.
Kipimo hiki hufanywa na daktari bingwa akisaidiana na madaktari wengine na manesi wa kitengo. Wataalamu hawa wa endoscopy walipokea mafunzo kutoka kwa wataalamu kutoka Ujerumani, pia baadhi yao walipelekwa katika hospitali ya taifa Muhimbili kujifunza utaalamu zaidi. 

Baadhi ya maradhi ambayo tunayagundua kwa kipimo hiki ni pamoja na vidonda vya tumbo, mishipa itwayo Esophagial varices kitaalamu, kansa za koo, tumbo na za utumbo mkubwa.

Matibabu ambayo tunayafanya ni pamoja na kufunga mishipa hii iitwayo Esophagial varices na vidonda vya tumbo ambavyo husababisha mgonjwa kutapika damu, pia tunatoa vitu kama mifupa ya samaki, shilingi, na vitu vingine ambavyo humezwa kwa bahati mbaya.