Ndanda

Idara ya wagonjwa wa nje na wa Dharura

Takribani wagonjwa 200-300 kwa siku hupata huduma kupitia idara ya wagonjwa wa nje na Idara ya wagonjwa wa dharura. Mfumo wa Manchester Triage ndiyo unaotumika katika kuwahudumia wagonjwa hao. Idara yetu ya wagonjwa wa nje na wa dharura ina Madaktari wawili wa matibabu (MD), Madaktari wasaidizi wawili (AMO),Madaktari bingwa wanne na wauguzi watano. Wagonjwa wa Dharura hutibiwa mara moja na daktari wa matibabu (MD) chumba cha dharura, ambacho kina vifaa vya kutosha kama mashine ya  Oksijeni.mashine ya kunyonya uchafu,dawa za dharura nk.  

Madaktari wetu wanafanya kazi  masaa 24. Pia katika chumba cha dharura daktari anapatikana kila siku  masaa 24  bila kujali siku za mapumziko na sikukuu. Huduma za wagonjwa wa nje pia zinajumuisha wagonjwa wa kulipia daraja la kwanza na  wagonjwa wa bima. Tunatoa huduma maalum ya kliniki ya sukari,kliniki ya shinikizo la damu,kliniki ya ugonjwa wa mafigo,kliniki ya magonjwa ya akili na CTC. Pia kliniki za kitaalam zinapatikana kwa upande wa magonjwa ya moyo (Jumanne na Jumatano), ENT,pua,masikio na koo, (Jumanne na Jumatano) Dawa za ndani (kila siku). Magonjwa ya wanawake (kila siku), Upasuaji (kila siku),Madaktari wa watoto (kila siku) na magonjwa ya nephrology (Mara moja kwa mwezi).