Ndanda

CT Scan

Hosteli

Tangu miaka kadhaa, tuna mpango wa ujenzi wa hosteli kwa ajili ya madaktari tanajari na wafanyakazi wengine. Kutokana na eneo letu la kijiji, maduka ya binafsi kumekuwa na ukomo. Kwa viwango vya nyumba za kulala kwa afya, umeme na maji ni duni na wakati mwingine zimekuwa mbali  kutoka hospitali. Kwa upande mwingine idadi ya wafanyakazi kwenye taasisi yetu inaongezeka mwaka hadi mwaka. Mahitaji ya malazi kwa wafanyakazi wetu wa muda mfupi ni muhimu sana,Pamoja na wataalamu wanaotutembelea kutoka nje na  madaktari tanajari ambao wanafanyakazi mwaka mmoja.

Hosteli itajengwa kwa awamu upande wa pili wa barabara kuu. Hatua ya kwanza itakuwa ujenzi wa jengo moja ambalo litakuwa na vyumba 10 vya kujitegemea, mapokezi, jiko, eneo la  chakula na kuosha nguo. Jengo hili ni maalum kwa wageni wa hospitali ambao wanatembelea kutoka nje. Ujenzi wa jengo hili tayari umeanza mwezi wa tano 2023 na utakamilika mwishoni mwa mwaka huu. Hatua ya pili itakuwa ujenzi wa jengo lenye vyumba 14 maalum kwa ajili ya madaktari tanajari. Ujenzi wa majengo mengine ya wanachuo Ndanda COHAS na makundi mengine utafuata.