Ndanda

CT Scan

Makabidhiano ya Vyoo Wodi ya Magonjwa ya akina Mama, kabla na baada ya kuzaa

Mnamo tarehe 22 Machi  2023, vyoo vipya vya wodi ya magonjwa ya akina mama, kabla na baada ya kuzaa vilivyofanyiwa ukarabati vilikabidhiwa. Mradi huu ulianza Mwezi wa kumi na mbili 2022. Ulikusudiwa kukarabati na kuboresha vyoo ambavyo ni rafiki kwa wasiojiweza, uboreshaji wa usafi na kuwa na nafasi zaidi kwa mama zetu wa kabla na baada ya kuzaa kwa kuzingatia faragha.    

Ukarabati wa kina na umaliziaji nzuri umeleta mwonekano wa kuvutia na wa kisasa wa vyoo. Walemavu wataweza kuingia na kutumia kwa urahisi, vyumba vimeundwa na vifaa vya kisasa vimefungwa. Uhakika wa usambazaji wa maji safi upo, mfumo wa maji taka upo vizuri pia. Uboreshaji wa usafi na faragha umezingatiwa. Ukarabati wa sehemu ya  kuosha nguo  kwa ajili ya akina mama wa wodi ya kabla na baada ya kuzaa wenye uhitaji wa kuosha nguo umezingatiwa. Wafanyakazi na wagonjwa wetu tunawashukuru sana wafadhili wetu kwa kufadhili miradi hii katika hospitali yetu.