Ndanda

Sherehe ya Kubariki mfumo wa Umeme wa jua

Tarehe 11.09. 2023 Mradi wetu wa umeme wa jua ulizinduliwa kwa kubarikiwa na Abate Emmanuel kutoka Abasia ya Uznach, Switzerland na Abate Romain kutoka Agbang, Togo.  Mradi ulijumuishwa na uwekaji wa paneli za umeme wa jua zenye kWp 300, betri yenye kWh 399 kwa ushirikiano wa mtambo wa umeme wa maji na jenereta mpya yenye ufanisi.               

Wakati wa mchana  umeme wa jua unatumika maeneo yote. Jioni na usiku mfumo wa umeme wa maji utasambaza kote. Betri huimarisha mfumo kwa kulipiza umeme ukishuka, kwa mfano wakati wa mawingu kupita, jenereta uhitajika kwa matumizi. wakati mifumo mingine haiwezi kutoa nguvu ya kutosha, kwa mfano mvua inaponyesha siku nzima. Msimu wa kiangazi kwa asilimia mia moja ya hospitali na na mahitaji ya Abasia yatajitosheleza na mfumo huu wa nishati mbadala. Ndani ya msimu wa mvua umeme wa jua utatoa nguvu kidogo na umeme wa maji zaidi. Hata hivyo, jenereta itahitajika mara chache tu. Mradi huu mkubwa na muhimu uliogharimu kiasi cha €800,000 umewezekana kwa misaada kutoka Abasia ya Uznach, (Switzerland) Abasia ya Schuyler USA na BEGECA (Germany)