Ndanda

Makabidhiano ya Upanuzi wa Ndanda COHAS

Mnamo tarehe  08/11/2022, Makabidhiano ya Upanuzi wa Chuo cha Ndanda cha afya na sayansi shirikishi (Ndanda COHAS) ilifanyika. Kutokana na uhaba wa vyumba vya madarasa pamoja na vyumba vya kufanyia kazi zingine, tumefanikisha upanuzi wa chuo chetu kupitia ujenzi wa jengo jipya lenye ghorofa moja. Ujenzi ulianza mwezi wa tano 2022 na umekamilika ndani ya miezi sita kama ulivyopangwa.

Jengo jipya limejengwa karibu na jiko la chuo lenye bwalo la chakula kwa wanachuo wasiozidi 220 katika sakafu ya chini, na kwenye ghorofa ya kwanza kuna maabara ya kompyuta na maktaba. Vyumba ambavyo vilitumika kwa ajili ya maabara ya kompyuta na maktaba hapo awali, kwa sasa vinaweza kutumika kama madarasa.