Ndanda

Ujirani mwema

Mnamo tarehe 21.8.2021, Tuliandaa mkutano wa ujirani mwema na wawakilishi watoa huduma wa afya wa mkoa wa Mtwara na Lindi.
Lengo lilikua kuimarisha uhusiano mzuri na vituo vya afya na zahanati, kutoa habari juu ya huduma zinayopatikana katika taasisi yetu.
Washiriki 44 kutoka mikoa ya Mtwara na Lindi walishiriki, pamoja na Mganga mkuu wa mkoa wa Mtwara, Mganga Mkuu wa Wilaya ya Masasi, Mwenyekiti wa bodi ya ushauri ya hospitali na Mwenyekiti wa bodi ya wadhamini.

Uwasilishaji kuhusu huduma zinazopatikana katika kituo chetu ziliandaliwa na wakuu wa idara ya wagonjwa wa nje/Dharura,kitengo cha wagonjwa mahututi ,kitengo cha utunzaji mkubwa wa watoto wachanga, kitengo cha uchujaji damu,maabara,Tiba za mwili na mifupa.
Wshiriki walithamini kupata ufahamu wa kina juu ya huduma zinazotolewa na miradi iliyotekelezwa na mingine ambayo bado inaendelea.
Pia walitoa ushauri mzuri juu ya namna ya kuboresha huduma zetu na ushirikiano na vituo vya afya na zahanati