Ndanda

Mwenge wa Uhuru 2023

Tarehe 8 mwezi wa Nne 2023,  Msafara wa mbio za Mwenge wa Uhuru Tanzania 2023, ukiongozwa na Bw. Abdalla Shaib Kaim ulizindua rasmi jengo letu la kutoa huduma za dharura,Idara ya wagonjwa wa nje na Utawala. Kwa sasa jengo limefunguliwa kwa ajili ya kutoa huduma na wagonjwa wetu wanafaidika na huduma bora za dharura na kutumia muda mfupi kwa matibabu kwa wagonjwa wa nje kwa umakini mkubwa bila msongamano. Mwenge wa Uhuru ni tukio la kitaifa tangu Tanzania ipate Uhuru mwaka 1961. Kila mwaka huzungushwa nchi nzima kwasababu ya kuonyesha ari ya Uhuru na kutumika kwa ajili ya kukagua miradi iliyokamilika, inayoendelea ambayo inachangia moja kwa moja katika jamii na kwa umma kwa ujumla.

Kukamilika kwa wakati na kwa mafanikio kwa mradi wa jengo la Dharura, Opd na jengo la Utawala kumeipa hospitali yetu fursa ya kutambuliwa kwa kuja kwa Msafara wa mbio za Mwenge wa Uhuru 2023. Kwa sababu ya ubora wa mradi huu kwa umma bila kujali umiliki binafsi wa hospitali. Uongozi na wafanyakazi wa hospitali ya Mtakatifu Benedicto Ndanda inawashukuru sana wafadhili wetu kwa kufadhili miradi mbalimbali katika hospitali yetu, Serikali ya Tanzania kwa misaada kadhaa na kamati ya Mwenge wa Uhuru kwa kutambua juhudi zetu bila kuchoka katika kuboresha huduma za afya ambazo zinapatikana kwa wote.

Angalia video kupitia linki hii.