Ndanda

Daktari wa mishipa ya damu

Tarehe 8/5/2021 hadi 10/5/2021, Dkt. Wambura Boniphace Wandwi kutoka Dar es Salaam alitutembelea Ndanda hospitali. Ilikuwa ziara ya pili, mara ya kwanza alitutembelea mwezi wa pili mwaka 2021. Lengo lilikuwa kuwaona wagonjwa wetu wa dialysis ambao wanahitaji operesheni ya fistula ama kuwekwa katheta inayoweza kukaa muda mrefu.
Hadi sasa, wagonjwa wetu wengi wa dialysis wamekuwa wakihudumiwa kupitia katheta za muda. Suluhisho ni kupata fistula – yaani kukatwa kwa muda mrefu kati ya mshipa mkubwa au  mshipa mdogo wa mkono. Wengine ambao hawafit kwa operesheni ya fistula wanaweza kupata katheta za muda mrefu. 

Jumamosi tarehe 8/5/2021, Dr. Wandwi alifanikiwa kufanya operesheni 5 za fistula na kuweka katheta za muda kwa wagonjwa wawili. Jumapili, tarehe 9/8/2021, alifanya operesheni za fistula 3 na kuweka katheta za muda 3.
Alipotutembelea mara ya kwanza mwezi wa pili, Dr. Wandwi ameshafanya operesheni za fistula kwa wagonjwa 13. 
Haya ni mafanikio makubwa kwa wagonjwa wetu wa dialysis kwani sasa wanaweza kuendelea na huduma ya dialysis bila hatari ya maambukizi.