Ndanda

Wataalamu wapya

Asante kwa ushirikiano na Hospitali ya Taifa Muhimbili (MNH) na Taasisi ya mifupa Muhimbili (MOI) Madaktari bingwa wapya wanatutembelea Ndanda mara kwa mara kuanzia mwezi wa sita mwaka 2022. Wanashughulikia magonjwa ya ngozi, Moyo, Masikio, pua na  koo, Magonjwa ya akina mama, utaalamu wa dawa ya usingizi, upasuaji wa midomo na mifupa ya taya, upasuaji wa mishipa ya fahamu. Pia tunashirikiana na mtaalamu wa magonjwa ya njia ya mkojo, ambaye anatutembelea kwa makubaliano kati yake na hospitali ya Ndanda. Wataalamu hao hututembelea kwa siku kadhaa kwa kila mwezi kulingana na upatikanaji  wao na mahitaji ya taasisi yetu. Pia tuna mtaalamu wa Lishe na daktari bingwa wa  mifupa na viungo bandia ambao wanatutembelea kutoka Taasisi ya mifupa ya Muhimbili wiki ya kwanza na ya pili ya kila mwezi. 

Mahitaji  ya huduma hizi ni kubwa sana. Wagonjwa wengi kutoka vijijini,hasa watoto,wanahitaji ushauri wa mtaalamu wa magonjwa ya ngozi. Wakati wa uchunguzi katika shule za msingi tumeona kuwa asilimia 70 hadi 80 ya watoto wengi wana maambukizi ya fangasi, pia kwa upande wa magonjwa ya masikio, pua na koo na magonjwa ya moyo. Daktari bingwa wa upasuaji wa midomo na mifupa ya taya anafanya upasuaji uliokuwa mgumu, kwa mfano wagonjwa waliovunjika sana usoni Daktari bingwa wa upasuaji wa mishipa ya fahamu (Prof.Dk. Kahamba) anafanya upasuaji wa mishipa ya fahamu kwa wagonjwa wanaovuja damu ndani ya kichwa au uvimbe. Uwepo wa mtaalamu wa lishe una thamani kubwa kwa wagonjwa wetu wa kliniki za kisukari na shinikizo la damu, kitengo cha uchujaji damu,wagonjwa mahututi pamoja na wagonjwa wa wodi za watoto na wodi za kawaida na upasuaji. Mtaalamu wa mifupa na viungo bandia hutuwezesha kutengeneza viungo bandia vya hali ya juu.