Ndanda

Kubariki wodi mpya ya binafsi

Tarehe 29.04.2022 Abate Christian Temu OSB  aliongoza sherehe ya kubariki wodi mpya ya binafsi inayoitwa wodi ya Sr. Thekla ambaye ni mwazilishi wa hospitali hii mwaka 1928. Licha ya kuchelewa kukamilika kwa wakati mradi huu umetekelezwa kwa ubora zaidi na kutekelezwa kwa viwango vya kisasa,muonekano wa jengo unavutia kwa nje na ndani.           

Kwa mazingira yaliyopo yatatusaidia sana kutekeleza dhamira yetu ya kuponya wagonjwa kwa kutoa huduma bora zaidi za afya. Huduma zitatolewa kwa wote kwa gharama kati ya shilingi 40,000 na 100,000 kwa siku kulingana na mazingira yetu. Jengo lina vyumba 10 vya wagonjwa,vikiwemo vyumba 3 vya wagonjwa wawili,vyumba 6 vya mgonjwa mmoja mmoja na chumba kimoja cha VIP. Mahitaji ya huduma hii ni kubwa sana,hivyo tunatarajia kuwa na wagonjwa wengi wodi binafsi ambapo mapato yatakua makubwa ambayo yatatumika kwa kusaidia wagonjwa wa hali ya chini kwenye vijiji vilivyotuzunguka.