Kwa sasa kitengo cha wagonjwa wa nje hakina viwango vya kisasa katika kuwahudumia wagonjwa wa dharura. , hivyo tunapanga kujenga na kukarabati miundo mbinu iliyopo. Lengo ni kuwa na idara pekee ya dharura na kuboresha huduma kwa wagonjwa wa nje na kliniki maalum.Mwezi wa nane 2021,wataalam kutoka Hospitali ya Taifa ya Muhimbili walitutembelea na kutushauri namna ya uboreshaji wa mipango hiyo.
Wakati mgonjwa anaingia atapokelewa na dawati la habari, kutakuwa na uchunguzi wa kuona na kupima. Wagonjwa wa dharura wataingia idara ya dharura ambako kuna vyumba vya ufufuo,ukumbi wa dharura na vyumba vya matibabu. Wagonjwa wengine wataingia Idara ya wagonjwa wa nje watajiandikisha, watapimwa na kutambuliwa, vyumba vya daktari na kliniki maalum. Hii itaboresha huduma za dharura na kwa wagonjwa wengine wa nje kuzuia wagonjwa na jamaa kupoteza muda usio wa lazima. Kwa hiyo,wagonjwa wa nje na dharura watatibiwa kwa muda mdogo na kwa viwango kwa mujibu wa miongozo husika. Ujenzi umeanza Januari na huenda ukakamilika Septemba 2022.