Ndanda

Kitengo cha Endoskopia

Kitengo chetu cha endoscopia kina mashine za kisasa ambazo hutumia camera inayowezesha kuingia katika tumbo, utumbo mdogo na utumbo mkubwa, pia inatuwezesha kuingina ndani ya mapafu. Tunatumia minara miwili ya endoscopia yenye gastroskopia tano,kolonoskopia mbili na bronchoskopia moja. Huduma hizo hutolewa katika vyumba vipya vilivyofanyiwa ukarabati na mazingira mazuri kwa wagonjwa wetu na wafanyakazi wetu. Endoskopia hufanywa na mtaalam mmoja na timu yake,inayojumuisha madaktari wawili wa matibabu (MD) na wauguzi 6 wa endoscopy. Timu hiyo ilipata mafunzo na wataalam wakuu kutoka Ujerumani. Wengine wamepata mafunzo Idara ya Endoscopy ya Hospitali ya Taifa Muhimbili Dar Es salaam. 

Tunatumia endoscopy ya kisasa ya video ambayo ina uwezo wa kufanya uchunguzi na taratibu mbalimbali wakati wa huduma. Taratibu hufanywa na dawa ya usingizi ya muda mfupi. Baadhi ya magonjwa tunayoyagundua  ni pamoja na ugonjwa wamaambukizi ya tumbo, vidonda vya tumbo, mishipa ya koo au tumbo, Kansa ya tumbo na utumbo.  Huduma zitolewazo baada ya kugunduliwa, kuondoa kitu kisicho hitajika mwilini, matibabu ya wagonjwa wenye matatizo ya kumeza au kutapika damu  na matibabu ya wagonjwa wenye hatua ya kwanza ya kansa. Idadi ya endoskopies zilizofanywa katika hospitali yetu imeongezeka kutoka 187 mwaka 2018 hadi 1358 mwaka 2023. Mahitaji ya uchunguzi huu ni muhimu sana  kwasababu taasisi yetu inatoa huduma hizi maalum katika ukanda wa kusini mwa Tanzania.