Ndanda

Vitanda vipya

Shukrani kwa mchango wa wafadhiri, tumepokea vitanda 40 vya hospitali mwezi Januari 2021.
Vitanda hivyo vimetolewa kwa msaada toka hospitali za Mindelheim na Ottobeuren huko Bavaria, Ujerumani na vimesafirishwa kuja Ndanda katika makontena 2. Vitanda hivzo viko kwenye ubora na katika hali nzuri. 

Vitanda hivi vitabadilishwa na vitanda vya yamani ambavyo havikuwa na mataili  kwenye wodi zetu. Pia tumepokea magodoro na magogo.
Msaada huo umefadhiriwa na wataalamu wetu Waandamizi na usafiri wa vitanda hivyo umedhaminiwa na KONRAD KLEINER GmbH, Mindelheim, Ujerumani.
Asante sana kwa mchango huu, ambao utakuwa msaada kwa wagonjwa wetu kwa miaka mingi!