Ndanda

Upasuaji na urekebishaji wa viungo

Kambi na Mradi wa Interplast hufanywa kila mwaka katika Hospitali ya Mt benediktine Ndanda,ikishirikisha wataalamu mbalimbali wa upasuaji, watoa dawa ya usingizi na manesi kutoka Ujerumani wakishirikiana na madaktari na manesi wazawa.Upasuaji ulifanyika kuanzia mwezi wa kumi(Oktoba) tarehe 25 hadi tarehe 8 ya Mwezi wa kuminamoja( Novemba) Mwaka 2019.

Kwa kipindi hicho, jumla ya watoto 36 na watu wazima 21 walipata huduma ya upasuaji.

Wagonjwa wote wenye matatizo ya mdomo wa sungura walirekebishwa,na wale waliopata matatizo ya viungo baada ya kuungua na moto ama makovu walipatiwa unafuu wa tiba ya upasuaji kwa marekebisho, hudumua hii yapaswa kuendelezwa kwani inamanufaa makubwa kwenye jamii yetu.

Gharama za upasuaji,malazi,na chakula ni bure kwa wagonjwa wetu.