Ndanda

Kambi ya mtoto wa Jicho 2023

Daktari Winfried Grasbon, mtaalamu wa macho kutoka Ujerumani alitutembelea kwa mara nyingine Ndanda kuanzia tarehe 07/03/2023 hadi tarehe 14/03/2023. Ni mara ya sita Ndanda na ya mia moja na mbili Tanzania. Kama kawaida alisaidiwa na timu yake ya  wauguzi wazawa pamoja na wafanyakazi wetu wa Idara ya macho, wakiongozwa na daktari bingwa wetu wa macho daktari Hussein Mjaliwa, ambaye amemaliza taaluma yake Dar es Salaam mwishoni mwa mwaka 2022. Kurudi kwa daktari Mjaliwa inatuhakikishia  kuendelea kutoa huduma za kibingwa katika idara ya macho kwa wagonjwa wetu pamoja na upasuaji wa mtoto wa jicho.                   

Wagonjwa wengi wamekuja wakiwa na  hatua ya mwisho ya mtoto wa jicho iliyosababisha kutoona vizuri  au  upofu. Wakati wa kambi hiyo  Daktari  Grasbon na timu yake wamefanikiwa kufanya upasuaji wa mtoto wa jicho kwa wagonjwa sitini ndani ya wiki moja. Wagonjwa walichangia shilingi laki moja na elfu hamsini (150,000) kwa ajili ya Upasuaji, chakula na kulazwa. Baada ya wagonjwa kufanyiwa upasuaji wanaona tena kama kawaida. Licha ya kutibu wagonjwa, wafanyakazi wetu wameweza kujifunza zaidi. Daktari Grasbon pia ametoa msaada wa vifaa mbalimbali vya thamani kwa ajili ya idara ya macho kupitia shirika linaloitwa Blindenhilfe Hettensshausen. Vifaa hivyo vitawezesha kutoa huduma bora kwa wagonjwa wetu kwa gharama nafuu. Kujitoa kwa Daktari Grasbon ni kwa ajabu na kuvutia ukizingatia ana umri usiopungua miaka themanini na nne (84)