Kuanzia tarehe 19/03/2023 hadi tarehe 02/04/2023, Daktari Ute Terheggen na timu yake walitutembela Ndanda. Ni wataalamu maalum wa upasuaji wa mguu kifundo uliodharauliwa. Watoto walio na mguu kifundo wanaweza kutibiwa kwa kufunga kopa, ikiwa matibabu yataanza mapema siku chache au wiki baada ya kuzaliwa. Kwa wanaokuja wakiwa wamechelewa sana kwa njia hii ya kufunga kopa wanapaswa kutibiwa kwa upasuaji maalumu. Matangazo kuhusu kambi hii yalifanywa kupitia vipeperushi na matangazo ya redio. Zaidi ya Wagonjwa 70 walifika na wote walipewa ushauri na wataalamu.
Madaktari 4 wa upasuaji wa mifupa, wataalamu wa usingizi wawili, wauguzi wawili wa chumba cha upasuaji na muuguzi mmoja wa dawa ya usingizi kutoka Ujerumani. walishirikiana na wafanyakazi wetu. Wamefanikiwa kufanya upasuaji wa kwa wagonjwa 35 bila matatizo yeyote. Baada ya muda wa upasuaji wagonjwa wataanza kutembea kama kawaida. Mradi huu umefadhiliwa na shirika la misaada linaloitwa Pro Interplast na huduma zote za upasuaji unafanywa bure bila malipo,ikiwemo kulazwa na chakula kwa wagonjwa.