Wodi zetu zilijengwa kati ya mwaka 1965 na 1970. Kwa sasa hazikidhi mahitaji na viwango, madirisha yameharibika ,sehemu za paa zinavuja maji inyeshapo mvua,wagonjwa kukosa faragha, vyoo si rafiki kwa wenye ulemavu n.k. Ukararabati unahitajika kwa haraka, pamoja na mabomba ya maji ya mvua,ukarabati wa korido na ujenzi wa vyoo rafiki kwa wenye ulemavu.
Kuanzia Septemba hadi Desemba 2021, tumefanikiwa kukarabati wodi yetu ya mifupa ya wanaume na korido. Mwezi Septemba 2022, tumekamilisha ukarabati wa wodi ya wanaume na Januari 2023 tumemaliza ukarabati wa wodi ya wanawake. Faragha kwa wagonjwa imepatikana kupitia uwekaji wa mapanzia. Vitanda vyote kuna mfumo wa oksijeni ambao umefungwa na mfumo wa simu kwa ajili ya mawasiliano na wauguzi. Katikati ya wodi kuna mahali wanapokaa wauguzi kwa ajili ya uangalizi wa karibu kwa wagonjwa. Vyoo vyote vya wodini vimejengwa kati ya Septemba 2021 na Septemba 2023. Mwezi Juni 2023 tumeanza ukarabati wa wodi ya upasuaji wa jumla ya wanaume ukarabati utakamilika Mwezi Septemba. Baada ya hapo wodi ya wajawazito itarekebishwa.