Ndanda

Kambi ya  Madaktari Bingwa wa Upasuaji 2021

Kambi ya Madaktari bingwa ni mradi unaofanywa kila mwaka katika hospitali ya Mtakatifu Benedicto Ndanda kwa ushirikiano wa timu ya madaktari bingwa wa upasuaji,watoa dawa ya usingizi na wauguzi wa kutoka Ujerumani na madaktari na wauguzi wetu. Mwaka huu 2021 upasuaji umefanyika kutoka tarehe 24 mwezi wa 10 hadi tarehe 6 mwezi wa kumi na moja. Wagonjwa walio na matatizo ya  midomo sungura,saratani ya ngozi,mikazo na ulemavu mwingine walihimizwa kuja katika kituo chetu kupitia mabango na matangazo ya redio.

 Zaidi ya wagonjwa 108 walifika katika kambi hii, na wote walifanyiwa uchunguzi na madaktari bingwa wa upasuaji. Wagonjwa 71 walifaa kwa matibabu maalum na zaidi ya huduma 130 zilifanyika kwa mafanikio. Wagonjwa wengine walipata upasuaji zaidi ya moja. Huduma hizo zilitekelezwa kwa ushirikiano wa karibu na wafanyakazi wetu, mafunzo ya kina yalitolewa na wataalam kwa madaktari na wauguzi wetu.  Wagonjwa wetu wamepata faida kubwa na wamethamini mno huduma walizopata.  Huduma zote pamoja na kulazwa, dawa na chakula ziltolewa bure kwa wagonjwa wetu.