Ndanda

CT Scan

Kituo cha Huduma ya Mama na Mtoto

Miundombinu ya kliniki ya watoto katika hospitali yetu, pamoja na  wodi ya akina mama na uzazi, ina zaidi ya miaka 50 na ukarabati umekuwa ukicheleweshwa. Kitengo cha huduma maalum kwa watoto wachanga (NICU), ambacho kimejengwa mwaka 2020, kina manufaa makubwa kwa wagonjwa wetu, na kutokana na mahitaji makubwa vyumba vimekuwa kidogo kwa sasa. Zaidi ya hayo, huduma hizi kwa ajili ya akina mama na watoto zinapatikana sehemu tofauti ndani ya hospitali. Kwa hiyo wakati wa warsha mbunifu wetu wa majengo mwezi wa kumi na mbili 2022, tulichora ramani ya kituo cha mama na mtoto, ambacho kitashughulikia huduma zote zilizotajwa hapo juu katika sehemu moja ya hospitali.                              

Tunapanga  ukarabati  thabiti wa miundo mbinu ya kisasa ya wodi yetu ya watoto na kuongeza sehemu za Huduma za Kitengo cha huduma maalum kwa watoto wachanga (NICU), Kitengo cha Huduma maalum kwa watoto (PICU), wodi ya uzazi na wodi ya akina mama. Mbali na vyumba vya wagonjwa, kila eneo lililotajwa hapo juu litakuwa na eneo la mapokezi, vyumba vya madaktari na vyumba vya uchunguzi. Kuna mpango wa kujenga chumba cha upasuaji kwenye wodi ya uzazi na pia vyumba vya tiba na mikutano kwenye wodi ya watoto. Aidha, tutatoa mafunzo jikoni  kwa akina mama wenye watoto wenye utapiamlo jinsi ya kuandaa mlo wenye lishe bora.