Ndanda

Kambi ya Afya ya Kinywa na Meno 

Kuanzia tarehe 23.05.2022 hadi tarehe 26.05.2022,tulikuwa na kambi ya afya ya kinywa na meno kwenye kituo chetu. Madaktari ishirini wa upasuaji wa afya ya kinywa na meno kutoka sehemu mbalimbali za Tanzania walitutembelea kwa ajili ya kufanya uchunguzi na matibabu ya kinywa na meno. Uchunguzi wa jumla ulifanywa kwenye hema lililoandaliwa karibu na hospitali. Baadhi ya madaktari wa afya ya kinywa na meno walikwenda shule mbalimbali za msingi na watoto wenye mahitaji maalum kama albino,walemavu na watoto vipofu ndani ya eneo la kilometa 100 kuzunguka Ndanda. Watoto na watu wazima wote waliotambuliwa kuwa na matatizo ya afya ya kinywa na meno walihimizwa kwenda kliniki ya afya ya kinywa na meno.

Jumla ya watoto 727 walichunguzwa kati ya asilimia 70 na 80 walikuwa na matatizo ya meno. Watoto wengi walikuwa na hali duni ya usafi wa kinywa na meno na baadhi yao walikutwa na matatizo mengine kama vile mdomo sungura. Kwa wote walipendekezwa kupata matibabu. Asante kwa mradi wetu wa msamaha wa watoto ;tunaweza kutoa matibabu kwa watoto maskini bila malipo. Wateja 120 wengi wao walikuwa watu wazima ambao waliripotiwa kuchunguzwa kwenye hema. Wateja 116 walitibiwa katika kliniki yetu ya afya ya kinywa na meno.Kwa ujumla hii ilikuwa na mafanikio makubwa na ni matumaini yetu kuwa wataalamu hawa watatutembelea tena mwaka ujao.