Tunatoa huduma bora katika hospitali yetu. Timu yetu ya Idara ya magonjwa ya ndani inajumuisha madaktari bingwa wawili, madaktari saba, msaidizi wa daktari mmoja na madaktari tanajari watatu. Tunatoa huduma za wagonjwa wa nje katika Idara yetu ya magonjwa ya ndani ambapo wagonjwa wa shinikizo la damu, kisukari, magonjwa ya moyo, figo,kupumua au maambukizi ya tumbo na utumbo na magonjwa mengine hutibiwa kwa mujibu wa miongozo ya kitaifa na kimataifa.
Wagonjwa waliolazwa hutibiwa katika wodi ya magonjwa ya ndani ya wanawake na wanaume. Wagonjwa wanaonwa na madaktari mara mbili kwa siku na mara mbili kwa wiki uonwa na madaktari bingwa. Wagonjwa waliozidiwa wanaangaliwa sehemu maalum wodini au wodi ya uangalizi wa karibu. (ICU) Uchunguzi wa ugunduzi unafanywa kwa umakini kwenye vipimo vya maabara, CTScan, ultrasound, echocardiography, X-ray na ECG. Uchunguzi maalum kama kipimo cha kamera (endoscopia), holter ECG, Stres ECG na ambulatory Bp (kwa saa 24) pia inapatikana. Matibabu yenye wigo mpana wa dawa, taratibu kama kutoa maji maji pembeni mwa mapafu /moyo au tumboni, taratibu za endoscopia na uchujaji damu hutolewa kulingana na hali ya mgonjwa.