Ndanda

Chuo cha Uuguzi

Dira

Kuimarisha afya na maisha bora ya mtu mmoja mmoja na jamii.

Dhamira

Kuwa kinara katika kuwapa mafunzo wauguzi ambao watatoa huduma bora za kiafya kwa mtu mmoja mmoja na jamii kwa Ujumla kupitia elimu ya uuguzi, mazoezi na utafiti.

Tunu

  1. Kuheshimu, kulinda na kukuza maisha ya mwanadamu kutoka kutungwa kwa mimba hadi kifo cha asili.

  2. Kufanya kazi kwa moyo, kujitolea, nidhamu, kujithamini, huduma bora, upendo na heshima kwa wagonjwa

  3. Kuhudumia wagonjwa wote kwa usawa bila kujali utaifa, elimu, kabila, dini, jinsia, hali ya kijamii na kiuchumi na maumbile