Ndanda

Blood donation and check-up at Nangoo village.

Siku ya Wagonjwa Duniani

Mwaka huu, siku ya wagonjwa duniani kanisa katoliki imesheherekea tarehe 11 Februari 2024. Hospitali yetu iliandaa kambi za uhamasishaji wiki mzima kwa kutoa huduma za afya kwa jamii husika. Dhumuni la tukio hili ni kuwafikia wakazi wa vijiji Jirani, kufanya uchunguzi wa afya, vipimo na fursa ya kuchangia damu kwa hiari. Kambi saba za uhamasishaji zilfanyika katika jamii tofauti za Jirani karibu na hospitali kuanzia tarehe 5 hadi 11 Februari 2024, ambapo tulifanya uchunguzi wa afya kwa kupima shinikizo la damu, sukari, HIV na ugonjwa wa ini. Huduma zote zilitolewa bila malipo kwa watu wote.

Jumla ya wakazi 265 walikuja kwa uchunguzi watu 78 waligundulika kuwa na shinikizo la damu (29%) Kisukri katika watu 7 (3%) na mmoja aligundulika kuwa na HIV. Wote waliokuwa na matokeo yasiyo ya kawaida walipewa ushauri nasaha kwa ajili ya kupata matibabu. Zilichangiwa Jumla ya chupa za damu 208. Kampeni za kuchangia damu ni muhimu sana kwa hospitali yetu, kwasababu mara nyingi tunakabiliwa na uhaba wad amu katika hakiba ya damu. Kampeni hizi ni muhimu kwa Maisha ya wagonjwa wetu hospitalini. Wakati huo huo zinachochea hisia ya mshikamano na wagonjwa miongoni mwa jamii katika vijiji Jirani.