Ndanda

Makabidhiano ya kliniki ya Macho, Kinywa na Meno

Mnamo tarehe 28.12.2023 yalifanyika makabidhiano ya ukarabati wa kliniki ya macho na kliniki ya kinywa na meno. Jengo lilijengwa miaka ya 1970 na ukarabati haukufanyika. Nafasi ndani ya jengo ilikuwa haitoshi haswa katika chumba cha matibabu ya kliniki ya kinywa na meno, mapokezi na sehemu ya kusubiri wagonjwa na vyoo vilikosekana kwa vitengo vyote viwili. Tumefanikiwa kufanya ukarabati wa kina kutokana na jengo lililopo kwa kuongeza vyumba katika kliniki ya kinywa na meno, sehemu mpya za kuingilia, mapokezi na eneo la kusubiri kupata huduma kwa kliniki zote mbili.

Madirisha mapya ya vioo na vigae vya sakafu vimewekwa katika vyumba vyote. Milango imebadilishwa, vyumba vyote vimepakwa rangi na kufungwa taa za kisasa (LED) Maeneo yameundwa upya na kutenganishwa. Mpangilio mpya unafanya kazi na vyumba vinaonekana kama vipya. Tunashukuru sana kwa mkutano wa wakilishi Abasia ya Uznach (USWIZI) pamoja na wafadhili binafsi ambao wamefanikisha mradi huu kwa ukarimu wao wa msaada wa kifedha.