Ndanda

CT Scan

Kambi ya Interplast  2023

Kuanzia tarehe  5 hadi 15  Novemba 2023, Dr. Daniel Tilkorn na timu yake ya madaktari wa Interplast, watoa dawa ya usingizi na wauguzi wa chumba cha upasuaji kutoka Ujerumani walitembelea hospitali yetu kwa mara ya sita. Kambi ya mwaka huu imepata mafanikio makubwa ya kurejea kwa wagonjwa na huduma zilizotolewa, ambazo zimebadilisha sana maisha ya wateja wengi wa kambi hiyo. Kabla ya kuanza kambi timu yetu ya madaktari,wauguzi na wataalamu wa tiba ya viungo  walifanikiwa kutangaza habari kuhusu kambi hii kupitia kwenye redio,mabango na mitandao ya kijamii.

 

Jumla ya wagonjwa 115 walifanyiwa uchunguzi na 74 walihitajika kufanyiwa upasuaji. Shida nyingi walizokuja nazo zilikuwa za moto kwenye maeneo tofauti mwilini ikiwemo vidoleni, kiwiko, mabega na magoti. Kutokana na madhara ya kuungua moto na ngozi kuvutika na kutofanya kazi kwa ufanisi wa viungo  wakati mwingine kushindwa kufumba macho ikiwa uso umeungua. Magonjwa mengine ambayo yamefanyiwa upasuaji ni pamoja na vidole vilivyoungana, ongezeko la vidole , midomo sungura na upandikizaji wa ngozi kwenye vidonda vilivyo kuwa wazi na kukata uvimbe. Huduma zote wakati wa kambi ikiwa pamoja na  upasuaji, dawa, malazi na chakula zilitolewa bila malipo kwa wagonjwa na jamaa mmoja. Uongozi, wafanyakazi na wagonjwa wamewashukuru sana Dr Daniel na timu yake kwa mchango mkubwa kwa kuwasaidia wagonjwa na wananchi maskini wa Tanzania.