Ndanda

Umeme wa Jua

Kutokana na ufungaji wa vifaa na mashine mbalimbali za kisasa katika hospitali yetu, kama mtambo wa kuzalisha oksijeni, mashine za uchujaji damu, vifaa mbalimbali chumba cha wagonjwa mahututi, CT SCAN, mtambo wa kujaza oksijeni,vifaa vya chumba cha dharura, kompyuta  nk. Kuna ongezeko kubwa la matumizi ya umeme. Vifaa vyote vinahitaji umeme thabiti bila kushuka kwa masafa ya nguvu ya umeme..   

Awali tulikuwa tunapata umeme wa maji. Nguvu yake ulikuwa 160kW  lakini mahitaji ya hospitali yalikuwa 220 kW (kuanzia Septemba 2023) Umeme wa  Jenereta ulikuwa unatumika zaidi. Kwa bahati nzuri sasa tumepata suluhisho endelevu kwa tatizo tulilokua nalo. Hii inajumuisha kwa ufungaji wa umeme wa jua wenye Kwp 300, betri yenye kWh 399 kwa ushirikiano wa umeme wa maji na jenereta mpya yenye ufanisi.

Mfumo wa udhibiti wa kielektroniki unahakikisha kwamba mahitaji wakati wa mchana umeme wa jua utatumika. Jioni na usiku umeme wa maji utatumika. Betri huimarisha mfumo kwa kulipiza umeme ukishuka. Wakati jua linawaka mzigo ni mdogo, ina chaji wakati wingu linapita mzigo unaongezeka ghafla na kutoa nishati inayohitajika. Jenereta hutumiwa wakati mifumo mingine haiwezi kutoa nguvu ya kutosha, kwa mfano wakati mvua inanyesha siku nzima.  Kwa kuwa upatikanaji wa maji na umeme katika maeneo mengi, Mradi wetu wa nishati Ndanda unaweza kuwa mfano katika bara la Afrika na kwingineko. Mradi huu mkubwa na muhimu, wenye thamani ya zaidi ya £800,000 umewezekana kwa misaada ya ukarimu kupitia Abasia ya Uznach na Schuyler pamoja na michango kutoka kwa BEGECA.