Kutokana na janga la kuenea kwa virusi vya Covid 19 duniani uongozi wa hospitali umeamua kujenga mtambo utakaozalisha hewa ya oxijeni.
Mradi huo ulianza mwezi Aprili na kukabidhiwa mtambo huo ulifanyika Septemba 2020.
Mmea hutoa hewa ya oksijeni na iliyofinyazwa kwa kitengo chetu kipya cha utunzaji mkubwa (ICU), dialysis, Kitengo cha Utunzaji mkubwa wa Watoto wachanga (NICU), ukumbi na uzazi.
Mtambo wa oksijeni utazalisha hewa itakayo tumika katika kitengo cha wagonjwa wanaohitaji uangalizi maalum, watoto wachanga wanaohitaji uangalizi maalum, chumba cha
upasuaji na wadi ya wazazi.hewa hii itasafirishwa kwa njia ya mabomba kutoka kwenye mitambo kwenda wodi husika.
Uwepo na upatikanaji wa oksijeni ni moja kati ya kigezo ili kuweza kufunga mashine itayosaidia wagonjwa kupumua (Artificial ventilation) katika ICU yetu. Hadi sasa kusini mwa Tanzania hakuna mashine hii, lakini tunatarajia kuwa na mashine tatu za kusaidia watu kupumua (ventilators) katika ICU yetu mpya.
Gharama za uzalishaji wa oksijeni katika mtambo huo ni shilingi 337.500.532. Mtambo huo utakuwa na nyumba ya jenereta, gharama za jengo na jenereta ni shilingi 67,481,764 za kitanzania. Gharama kuu ya mradi wote ni shilingi 404,982,296 za kitanzania. Mradi kwa jumla unategemea kukamilika mwezi wa nane mwaka 2020.