Ndanda

Fedha

„Kuelekea kwenye dhama ya kujitegemea na utoaji wa huduma bora zaidi katika hadhi ya juu.“

Ofisi ya hazina inamikakati malidhawa katika kuhakikisha ya kwamba mapato na matumizi ya Hospitali yanadhibitiwa pamoja na mali zisizoamishika vilivyo ili kulinda upotevu wa rasilimali hizo ili kuzidi kuendelea.

SHUGHULI ZA KIUHASIBU NA FEDHA

Kitengo kimeweka mkakati toka 2019 wa makusanyo ya mapato na matumizi kiofisi na pia wa kimanunuzi ya vifaa ili kukinga ubadhilifu.

Kitengo cha uhasibu kinashughulika na manunuzi pia kuhakikisha vifaa mbalimbali vinapatikana kwa matumizi ya hospitalini.

Pamoja na yote hospitali inajiendesha kwa hasara kutokana na mapungufu ya makusanyo ya mapato kuwa madogo.Hii pia inachangiwa na uelewa mdogo wa jamii inayoizunguka hospitali.

VYANZO VYA MAPATO

Vyanzo vikuu vya mapato ni kutokana na uchangiaji wa gharama za matibabu,ruzuku kutoka serikalini,pia kutoka Abasia ya Benedictine Ndanda,na Shirika la Mt Otillien, wahisani na marafiki mbalimbali.

SERA YA UCHANGIAJI

Hospitali inawakaribisha wahisani kwa kupitia miradi au ufadhili wa aina yeyote ile.

Yeyote mwenye nia anakaribishwa kuwasiliana nasi.

Mafunzo: hutegemea nafasi zikiwepo.

Mnunuzi: Fuatilia mlolongo wa manunuzi ya hospitali.

MFUMO WA KIUTAWALA: Huu usimamia taratibu zote za kiutawala kwa rasilimali watu na fedha ni mwomgozo malidhawa wa Kamati ya uendeshaji Hospitali (HMT) katika kujadili mipango na maamuzi ya kiutendaji.