Ndanda

Idara ya watoto

Idara ya watoto ina sehemu tatu 3 ambazo huwahudumia watoto yaani; Wagonjwa wa ndani, watoto ambao hawatimiza mwezi mmoja (noenatal) na wagonjwa wa nje yenye mjumuhisho wa huduma za Mama na Mtoto RCH ambayo hushughulikia watoto walio chini ya miaka mitano 5.

Idara hii ina Madaktari bingwa wawili 2, Daktari mmoja ambaye ni (MD),Madaktari 5 wanafunzi yaani Intern doctors,na manesi 22.Kitengo kinatoa huduma mbalimbali za kiuchunguzi kama vile Hematological, Biochemical, parasitogical, U/S, ECHO na X-rays.

Kitengo kimefaulu kushughulikia matatizo ya moyo na yale ambayo yanashindikana mgonjwa hupewa rufaa ya kwenda hospitali ya Taifa Muhimbili ama Hospitali ya ocean Road Dar es Salaam kwa matibabu zaidi.Pia wamefaulu kushughulikia matatizo machache kama Sphingolipidosis ambayo huitaji tiba maalum za enzaim (vichocheo).

Tunatoa shukrani na Asante kwa Mradi wa Msamaha wa Tiba kwa Watoto. Hivi sasa tunatoa huduma za msamaha kwa watot wenye wazazi wasio na uwezo wa kugharamia matibabu.