Ndanda

Team of Emergency Department

Idara ya dharura

Huduma za dharura hutibiwa haraka kwenye idara yetu ya dharura inayojitegemea yenye vifaa vyote vinavyohitajika. Uchunguzi unafanyika anapowasili mgonjwa. Kisha wagonjwa huletwa kwenye chumba kimojawapo cha kurejesha uhai kwa matibabu ya dharura au chumba cha matibabu. Chumba cha upasuaji wa dharura, chumba cha uangalizi na vyumba vya ziada vinapatikana. Huduma za dharura hutolewa masaa 24 kupitia timu yetu ya daktari mmoja, daktari msaidizi na wauguzi 6.

Baada ya kuwasili na kupima, wagonjwa hupata matibabu haraka na madaktari na wauguzi. Uchunguzi wa dharura kama vipimo vya haraka vya maabara, utrasound, kipimo cha moyo (ECG), hupimwa ndani ya Idara ya dharura. Ikihitajika mgonjwa kuonwa kwa wakati na mtaalamu wa idara. Matibabu ya dharura ya oksijeni, dawa na huduma ndogo zinatolewa ndani ya idara ya dharura. Mara mgonjwa anapoimarika hupelekwa wodi husika, chumba cha upasuaji au kuruhusiwa.