Ndanda

Blood donation and check-up at Nangoo village.

Wafanyakazi wa Kidini

Kama taasisi ya kidini, tuna nia ya kuimarisha roho ya kidini katika kituo chetu. Kwa hivyo, tunathamini uwepo wa wafanyakazi kutoka mashirika mbalimbali ya kidini. Hivi karibuni, idadi yao imeongezeka na kwa sasa tuna watumishi 25 wa kidini kutoka mashirika tofauti wakifanya kazi katika hospitali yetu.

Wako ma Brother 9 kutoka Ndanda Abbey wanaofanya kazi kama madaktari, kwenye idara ya utawala, maabara, na kitengo cha teknolojia na habari (IT). Masista 9 wa Shirika la Wabenediktini wa Kiafrika wa Mama Msaidizi wa Wakristo wanafanya kazi katika idara mbalimbali: Idara ya Meno, Huduma za Uuguzi, Maabara, Mapokezi, Duka la Dawa, na Idara ya Wagonjwa wa Nje (OPD). Masista 2 wa Shirika la Kimisionari la Wabenediktini wa Tutzing wanafanya kazi katika ofisi ya Uhasibu na kwenye stoo. Pia tunao Masista 5 kutoka Shirika la Masista wa Maria Mkingiwa Dhambi ya Asili (Mary Immaculate Sisters) huko Chikukwe. Wawili kati yao wanafanya kazi kama Maafisa wa Kliniki chini ya uangalizi wa madaktari Bingwa , na watatu kati yao wanafanya kazi kama matrons katika chuo chetu.