Mnamo tarehe 5 Mwezi wa kwanza mwaka 2024 Wodi ya Tibakemia ilikabidhiwa na mkandarasi. Tumeweza kurekebisha jengo ambalo halikuwa linatumika. Wagonjwa wanaweza kujiandikisha mapokezi na kupimwa vipimo vya awali katika chumba kimoja. Wagonjwa watakaa eneo la kusubiri hadi waitwe chumba cha daktari na daktari bingwa wa saratani . Daktari ataagiza dawa ambazo zimeandaliwa na mfamasia katika chumba maalum cha mtambo kinga. Kutoka hapo, dawa huletwa chumba cha matibabu kupitia eneo maalum lililojengwa
Wagonjwa hupokea dripu kwa njia ya mishipa ya damu kwa masaa kadhaa katika eneo la matibabu. Viti sita maalum vipo ambapo mgonjwa anaweza kukaa au kulala kwa raha wakati anapata huduma. Mnamo mwezi wa kumi na mbili 2023 baadhi ya wafanyakazi wetu walimaliza mafunzo ya Tibakemia. Tarehe 11 mwaka 2024 daktari wa magonjwa ya saratani kutoka Dar Es Salaam ametutembelea kwa mara ya kwanza na kuanza kutibu wagonjwa wa kwanza.