Tarehe 24/04/2023, Jengo la Idara mpya ya dharura,utawala, Idara ya wagonjwa wa nje pamoja na jengo la Ndanda (COHAS) lilizinduliwa rasmi kwa kubarikiwa. Ibada iliongozwa na Abate mstaafu Anastasius Reiser OSB na Br Tobias Dammert OSB, ambao walitutembelea kutoka nyumba ya misheni ya Wabenediktini Schuyler (Marekani) akiwemo mwenyeji wao Abate Christian Temu OSB wa Abasia ya Ndanda.
Idara mpya ya Dharura inafanya kazi kikamilifu. Ukiingia kuna dawati la huduma kwa wateja na vipimo vya awali, vyumba viwili vya ufufuo, chumba cha upasuaji wa dharura na vyumba vya matibabu. Kwa upande wa Idara ya huduma za wagonjwa wa nje OPD, mapokezi, huduma ya vipimo vya awali na vyumba 12 vya madaktari vikiwemo na kliniki za wataalam husika. Ghorofa ya kwanza kuna ofisi za utawala ambazo zinafanya kazi. Kwa nyongeza jengo jipya la Ndanda (COHAS) kuna bwalo la chakula kwa wanachuo 220, maabara ya komyuta na maktaba. Uongozi na wafanyakazi wa hospitali yetu inawashukuru sana wafadhili wetu kwa kuwezesha utekelezaji wa miradi hii.